Wanafunzi wa shule ya Sekondari Mbekenyera, iliyopo Kata ya Mbekenyera, wilayani Ruangwa, wamenufaika na huduma ya msaada wa kisheria waliyopewa kupitia Kampeni ya Mama Samia Legal Aid, iliyofanyika leo, Februari 25, 2025, shuleni hapo.
Timu ya wataalamu wa msaada wa kisheria imetoa elimu kuhusu sheria mbalimbali ikiwemo haki za mtoto, mapambano dhidi ya ukatili, na wajibu wa mtoto. Aidha, wanafunzi wamejifunza kuhusu umuhimu wa kulinda haki zao na namna ya kutafuta msaada wa kisheria endapo haki zao zitakiukwa.
Kwa upande wao, Wanafunzi hao wamesema kuwa elimu hiyo itawasaidia kujua haki zao na kujikinga dhidi ya ukatili na madhara mengine, huku wakisema kuwa ni muhimu kujua sheria za haki za binadamu na jinsi ya kuzitetea na kuzilinda kwa manufaa yao.
Kampeni ya Mama Samia Legal Aid inaendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kuelimisha wananchi, hasa vijana, kuhusu masuala ya kisheria na kuwawezesha kujua haki zao ili kuimarisha utawala bora na kuhakikisha haki inapatikana kwa wote.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa