Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Godfrey Zambi amewataka Wakurugenzi wakulipa mishahara ya watumishi kwa wakati wanaolipwa kwa fedha za mapato ya ndani.
Pia amewataka waajiri wa taasisi binafsi kuzingatia haki za wafanyakazi wao kwa kulipa maslahi ya wafanyakazi hao kwa wakati.
Ameyasema hayo leo Mei 1/2019 wakati wa maadhimisho ya mei mosi yaliyofanyika katika viwanja wa shule ya mpilipili Mkoani lindi mjini.
"Stahiki zipo nyingi ni wajibu wenu waajiri kutoa stahiki hizo anzeni na kuwapa vitendea kazi ili waweze kutimiza wajibu wao kama inavyotakiwa" amesema mheshimiwa Zambi.
Vile vile amewataka watumishi kuwa na imani na serikali ya awamu ya tano kwani inashughulikia na inaendeleza kusimamia haki za watumishi na zoezi la upandaji wa madaraja unaendelea.
"Rais wetu John Pombe Magufuli ni mtetezi wa haki za wanyonge anahakikisha kila mtu anapata stahiki yake fanyeni kazi mkiwa na imani na Rais kwani hatoacha kuwatimizia mahitaji yenu" amesema Zambi
Aidha amewataka wafanyakazi wa serikali na wataasisi binafsi kupinga vitendo vya rushwa katika maeneo yao ya kazi na ikitokea hali ya rushwa katika maeneo yenu ya kazi mpeleke malalamiko hayo katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa katika maeneo yenu ya kazi.
"Serikali ya sasa haitaki mchezo ukibainika unaomba au kupokea rushwa sitokuvumilia hatua kali za kisheria zitafuata kwa kufuata taratibu mtumishi kaa mbali na rushwa ni adui wa maendeleo "amesema Zambi
Wakurugenzi simamieni hivi vigezo cha mfanyakazi hodari ili watu waache kupeana tu kuwa kufuata nani mwaka jana kapata mwaka mwingine apate mwingine hata kama mtu amepata mara tatu na anasifa basi apate huyo huyo na si kupeana bila kuangalia vigezo muhimu.
Naye Mratibu wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi TUCTA bi Fatma Chiwonga amewaomba waajiri kuwasaidia wafanyakazi waliostaafu wanapata stahiki zao kwa wakati.
Pia ameiomba serikali kupunguza makato ya kodi kwa watumishi kutoka asilimia 9 mpaka asilimia 6 kwani kiwango cha makato ya sasa ni kikubwa sana.
"wafanyazi wanafanya kazi katika mazingira magumu tuwafanyieni unafuu hata kidogo haya makato kutokana na mishahara wanayopokea makato hayo yamekuwa ni makubwa" amesema bi Fatma.
Maadhimisho hayo kimkoa yamefanyika manspaa ya Lindi iliyopo Lindi mjini, Maadhimisho hayo yamebeba ujumbe wa "Tanzania ya uchumi wa kati inawezekana wakati wa mishahara na maslahi bora kwa wafanyakazi ni sasa"
MWISHO.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa