Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mhe.Selemani Mzee ambaye alimwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo wamewataka wananchi wa Mikoa ya Lindi na Mtwara kutotegemea zao moja la biashara kutokana na ardhi ya mikoa hiyo kustawisha aina nyingi za mazao.
Mzee ameyasema hayo alipokuwa akizindua Maonesho ya wakulima maarufu kama nane nane ya kanda ya kusini katika viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi.
Alisisitza kuwa kwa miaka ya hivi karibuni uzoefu na utafiti wa wataalam mbali mbali umeonesha kuwa kanda ya kusini kuna ardhi nzuri na rafiki kwa aina mbali mbali za mazao ya chakula na biashara ambayo huko nyuma hayakuwepo.
Alitaja baadhi ya mazao ya biashara ambayo yameonekana kustawi katika maeneo mengi ya Kusini ni pamoja na Ufuta,karanga, alizeti,choroko pamoja na mbaazi.
Mbali na hayo lakini pia Mhe.mgeni rasmi pia aliwasisitiza wananchi kuzingatia kilimo cha kisasa ili kupata mazao mengi na bora kwa ajii ya soko la ndani na nje ya nchi akitoa mfano wa zao la ufuta ambapo kwa msimu unaishia mwezi huu wa nane 2019 ambapo zaidi ya tani 60,000 za ufuta zimeshauzwa mpaka sasa ambapo kwa kiasi kikubwa zao hili linasafirishwa kwenda nje ya nchi.
‘’Mwaka huu mmefanya vizuri kwenye zao la ufuta ambapo Zaidi ya tani 60,000 zimeuzwa na kuingiza zaidi ya shilingi bilioni 160 zimeshapatikana kwa kipindi kifupi cha miezi miwili’’ aliongeza Mhe.Mzee.
Mhe.Mgeni rasmi pia aliwakumbusha wananchi wa baadhi ya maeneo yenye migogoro ya ardhi kuwa mpaka sasa katika mikoa ya Lindi na Mtwara sehemu ya ardhi inayotumiwa ni asilimia 26 tu na kiasi kinachobaki bado ni mapori na hivyo kuwaomba wananchi kila mmoja kuzingatia sharia,mipaka na mipango ya matumizi bora ya ardhi kama ilivyoainishwa, alisema ni ajabu kiongozi wa Wilaya au Mkoa kuitwa kusuluhisha mgogo wa ardhi huku kukiwa na mapori mengi katika maeneo yao.
Uzinduzi wa maonesho hayo yalihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Mkoa ya Lindi na Mtwara wakiwemo wakuu wa wilaya zote, wakurugenzi, wenyeviti wa halmashauri, madiwani pamoja na kamati ya ulinzii na usalama.
Manesho haya yanawajumuisha wataalam kutoka wilaya zote za kanda husika, taasisi mbalimbali za kilimo,ushirika na biashara pamoja na wananchi wanaotoka kwenye vikundi na mmoja mmoja kulingana na maeneo yao.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘’Kilimo, mifugo na uvuvi kwa ukuaji wa uchumi wa nchi”
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa