Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mhe, Rashidi Nakumbya imewataka wafugaji wakubwa waliovamia katika Wilaya hiyo kuondoka mara moja katika maeneo hayo walioweka kambi kwasasa kwasababu wameingia katika Wilaya ambayo haina eneo la kupokea wafugaji wakubwa.
Agizo hilo limetolewa leo tarehe 14/08/2019 kwenye kikao cha Baraza Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Rutesco Ruangwa mjini.
“Ieleweke siyo kuwa tunawakataa hawa wafugaji bila sababu tunasababu Wilaya ya Ruangwa inaeneo dogo ambalo linauwezo wa kupokea wafugaji mwenye ng’ombe kumi mpaka ishirini tu”
Aliendelea kusisitiza kuwa eneo kililopo ndani ya Wilaya ya Ruangwa kwa kilimo tu halitoshi hivyo hawawezi kupokea wafugaji wakubwa, wafugaji wakubwa na waliopo Wilayani humu waanze kuondoka mara moja na ameomba vyombo vya usalama vya Wilayani viwasaidie kuwaondoa wafugaji hao ambao wameishafanya mazungumzo nao sana.
Mhe. Nakumbya aliongeza kuwa ustaarabu na uvumilivu wa wakazi wa Ruangwa umekuwa unawafanya waonekane ni wadhaifu jambo linalowafanya wafugaji hao kuingiza mifugo yao kwa ubabe kwenye mashamba ya watu na kwa makusudi
“Msitulazimishe kushika mapanga kama nyie mnavyofanya, Ruangwa ni kisiwa cha amani ondokeni kwa amani hatuwaitaji katika eneo letu mliyoyafanya yanatosha ondoeni mifugo yenu atujawakaribisha mmevamia ondokeni mara moja”
Naye Diwani wa kata ya Matambalale Omari Liwikila alisema wafugaji wamekuwa wakitumia lugha mbaya na silaha jambo lililosababisha kujeruhiwa kwa mkazi mmoja kwenye kata ya Matambalale baada ya wafugaji hao kuvamia eneo hilo
Mheshimiwa Diwani alisema wafugaji hawa wamekuwa wanaingia kwa kuvamia na kusababisha maafa ya mazao na binaadamu bila kujali utu na katika kata hiyo mpaka sasa ni watu wa tatu wamefanyiwa vitendo hivyo vya ukatili na wafugaji hao.
Mhe,Liwikile alisema wafugaji hao wamekuwa wakilisha mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima wa Ruangwa huku wenyewe wakiishi kilwa hali inayosababisha wasipatikane pindi wanapotafutwa.
“Hivyo Mwenyekiti niombe Halmashauri yetu ifanye mazungumzo Na Halmashauri ya Kilwa iwadhibiti wafugaji wa eneo lao kwani madahara wanayoyaleta sasa watakuja kusababisha madhara makubwa zaidi hasa wanaoishi katika eneo la mto Mbwemkuru”
Baraza la Madiwani kwa pamoja liliazimia wafugaji hao waondoke mara moja katika Wilaya ya Ruangwa na waache kuingiza mifugo yao na kulishia katika mashamba ya wakazi wa Ruangwa
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa