Mwezeshaji wa mafunzo ya Utawala bora ndg, Uzima Justine amewaambia washiriki wa mafunzo wakayafanye mafunzo hayo yawe na tija na walichokipata wakakifanyie kazi.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na washiriki katika mafunzo ya Utawala Bora yaliyofanyika ukumbi wa Mkuu wa Wilaya Ruangwa mjini.
Ndg Justine alisema washiriki wakafanye kazi kwoa juhudi waache visingizio na watimizie wajibu wao kwa kufuata sheria na taratibu zote.
Aliendelea kusema mwanzo watendaji wa vijiji, wenyeviti wa vijiji na vitongoji walikuwa wanafanya kazi bila kujua wanapokosea hivyo waende wakafuate sheria za Utawala bora kama walivyofundishwa.
Aidha aliwataka kuhakikisha vijiji vyao vipo katika hali ya ulinzi, utulivu, amani na usalama Ili watu wawezi kufanya shughuli za uzalishaji mali.
Alisema wananchi hawezi kuzalisha mali kama kijiji hakina amani, utulivu na usalama hivyo wahakikishe amani azivunjwi ovyo kwani uzalishaji mali wa wananchi ni vyanzo vya mapato serikali ya kijiji.
Pia aliwataka wenyeviti wakijiji kuchukua hatua za kisheria kwa wahalifu waliopo maeneo yao baada ya kubainika kama ni wahalifu na wamefanya uhalifu.
Naye Mshiriki wa Mafunzo Mwenyekiti wa Kijiji cha Likangara Said Kauchumbe alisema anaishukuru taasisi ya CETA kwa kuwaletea mafunzo haya kwasababu yamewajenga na yamewapatia vitu vingi vya umuhimu.
Alisema Mwenyekiti walikuwa wanaongoza wananchi bila kufuata taratibu na walikuwa awajui makosa yao hivyo baada ya kupata mafunzo haya ni kama wamekuwa wapya katika uongozi wao.
Alisema anaomba uongozi wa Jukwaa la Elimu ya Uraia Tanzania (CETA) kuendelea kuwaletea mafunzo mengine ya kuweza kuwajengea uwezo katika kutenda kazi zao na pia CETA waweze kuwafikia viongozi wa serikali wa kijini wilayani kote Ruangwa.
Mafunzo haya yanahusisha Mwenyeviti wa vijiji, Watendaji wa Vijiji, na Wenyeviti wa kamati za kudumu za vijiji mpaka sasa mafunzo yametolewa kwa vijiji 44 na kata zote 22 na jumla ya washiriki waliopokea mafunzo hayo ni 355.
Mafunzo haya yatawafikia Mwenyeviti wa kijiji, Watendaji wa vijiji na Wenyeviti wa Kamati za kudumu za Vijiji wote walio ndani ya Ruangwa
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa