Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mheshimiwa Hassan Ngoma amewaagiza watendaji wa vijiji na waratibu elimu kata kuhakikisha mpaka tarehe 17/06/2022 wanafunzi ambao hawatafika shule pamoja na wazazi wao wachukuliwe hatua za kisheria.
Alisema kumekuwa na wimbi la watoto wengi vijijini kuacha shule au kuwa na utoro hali inayopelekea shule nyingi hapa Wilayani kuwa na utoro sugu.
Amesema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi tarehe 10/06/2022 aliyoifanya katika kijiji cha Lipande, Liugulu na Mchanamo Ruangwa.
"kila mzazi atimize wajibu wake jukumu la kupeleka mtoto shule ni wajibu wa kila mzazi kupeleka mtoto shule si hiari ni lazima.
"Mnadai haki zenu kwa serikali ila nyie kutimiza wajibu wenu amtaki sasa wazazi ambao hamtaki kutimiza wajibu wenu tutawashughulikia pamoja na hao watoto mnaokaa nao majumbani wakati wanahitajika shuleni" amesema Ngoma
Pia aliwataka wakulima wa ufuta kuacha kuuza kangomba na kuharibu ufuta kwa kutia michanga au mawe.
"Ruangwa tuna ufuta bora sana tukiutunza ufuta huo kwa bei za minada iliyofika sasa hivi Ruangwa tunaweza kuuza ufuta wetu kwa bei nzuri zaidi muhimu ni kutoharibu" amesema Ngoma.
Vilevile Mheshimiwa Ngoma aliwataka wananchi kujianda kwa zoezi la sensa ya watu na makazi ambalo linatarajiwa kufanyika tarehe 23/08/2022
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa