Uteuzi wa wagombea kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika 27 Novemba 2024 umefanyika rasmi leo, tarehe 8 Novemba 2024, na fomu zote za wagombea zimebandikwa kwenye maeneo mbalimbali ya Wilaya, wananchi wanahimizwa kutembelea vituo husika ambavyo fomu hizo zimewekwa ili kujiridhisha na majina ya wagombea.
Mchakato huo unalenga kutoa fursa kwa wananchi kukagua taarifa za wagombea na kujua wanaowania nafasi mbalimbali. Aidha, hatua hiyo inatoa nafasi kwa wananchi kutoa pingamizi dhidi ya wagombea ambao hawatimizi vigezo vilivyowekwa kisheria.
Afisa Uchaguzi wa Wilaya ya Ruangwa, Ndugu Charles Tamba, amesisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki kikamilifu katika ukaguzi huu ili kuhakikisha wagombea wanateuliwa kwa mujibu wa sheria na taratibu.
“Tunawaomba wananchi wasisite kutoa taarifa za pingamizi endapo kuna wagombea ambao wanadhani hawafai kushiriki uchaguzi huu,” amesisitiza Ndugu Tamba.
Ukaguzi huo wa fomu za wagombea ni hatua muhimu katika kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa haki na wa wazi, ambapo wananchi wanapata nafasi ya kuchangia na kuleta mabadiliko yenye tija.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa