Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mheshimiwa Hassan Ngoma amewataka watendaji walio na miradi ya ujenzi kuhakikisha miradi wanayotekeleza inaisha kwa wakati.
Ameyasema hayo wakati wa kikao cha baraza la madiwani cha robo ya tatu kilichofanyika tarehe 7 na 8/06/2022 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya
Mheshimiwa Ngoma alisema kuna miradi inayotarajiwa kukamilika tarehe 20 ya mwezi huu watendaji wanaosimamia miradi hiyo wafanye kazi ya ziada kuhakikisha inaisha kama inavyotakiwa.
"Nafanya ziara nikipita katika vijiji vyote watendaji simamieni miradi ikamilike, acheni maneno kinachoitajika ni utendaji".
Pia amewataka wananchi/madiwani wasimamie ufanisi na usalama wa miradi iliyo katika maeneo yao kwani ni wajibu wao kufanya ivyo.
"Acheni kurudi nyuma msitishwe na maneno ya watendaji wenye nia ovu, ni wajibu wenu kutembelea na kusimamia miradi katika maeneo yenu"amesema Ngoma
Aidha alisisitiza Waheshimiwa Madiwani kufanya mikutano ya vijiji katika maeneo yao ili kutatua changamoto katika maeneo yao.
"Nategemea ninapopita katika ziara zangu nikute mmefanya mikutano na mmeanza kutatua changamoto zilizopo katika maeneo yenu" alisema Ngoma
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Andrea Chikongwe alimpongeza mbunifu super mkuti kwa tunzo alizopokea na namna anavyofanya ubunifu wake.
Alisema Halmashauri itaangalia namna ya kumsaidia mbunifu huyo ili aweze kufanya vitu vizuri zaidi na kumtengenezea masoko ya bidhaa zake.
"Tutafuta masoko kwa ajili ya bidhaa anazotengeneza ila pia halmashauri iendele kuvumbua wabunifu wengine walio katika halmashauri hii" amesema Chikongwe
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa