Mkuu wa Mkoa ya Lindi Mhe. Zainabu Telack amesisitiza watumishi kufanya kazi kwa kushirikiana ili kufika malengo ya kuwahudumia wananchi kwa kufuata kanuni na taratibu.
Amesema hayo wakati wa kikao cha baraza la hoja leo tarehe 24/06/2022 kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya Ruangwa.
Amesema Mheshimiwa Zainabu kushirikiana katika kazi kutarahisisha utendaji kazi wa idara na vitengo na kuwezesha wananchi kupata huduma kwa wakati.
"Kila mtu ameajiriwa peke yake ila unapofika katika idara au kitengo unakutana na watu wengine, unapaswa ufanye nao kazi hatua kwa hatua na si kukwamishana" amesema Zainabu
"Wakuu wa idara shirikisheni kazi watu wenu wa chini msijilimbikizie kazi mkifanya hivyo mnachelewesha mambo ya serikali"
Pia amewataka watumishi kushirikiana kufunga hoja zote za mkaguzi wa nje ambazo bado hazijafungwa.
Aidha alisisitiza kuzingatiwa kwa taratibu za manunuzi na miongozo ya manunuzi, ikiwemo kuacha Wataalamu wa manunuzi wafanye kazi yao.
"Tuwaache wafanye kazi yao, tuache tabia ya kupita nyuma ya mgongo wao kwa sababu ni kuvunja sheria na ndio kunazalisha hoja za ukaguzi." Amesema Zainabu.
Mwisho
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa