"Tumetembea km 1500 kutoka Kaliua Tabora kujifunza mfumo wa stakabadhi ghalani Kwenye Wilaya ya mfano Ruangwa”
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya ya Kaliua Mhe. Dkt Gerald Mongella leo 16 Dec2024 wakati wa ziara ya kujifunza mfumo wa stakabadhi ghalani wilayani Ruangwa
“ Tumekuja kujifunza hapa maana tunapakuanzia kwakua sisi ndo wazalishaji wakubwa wa tumbaku Tanzania kwani tuna amcos 173 tutazitumia hizo kuanzisha mfumo huu kuwa tija katika jamii.”amesema Gerald Mongella
Naye mkurugenzi wa halmashauri ya Kaliua Jerry Mwaga amesema wameshawishika kujifunza mfumo huo baada ya kuona Halimashauri ya Wilaya ya Rungwa inanufaika na mapato pia mfumo huo kwao utasaidia kujua takwimu ya wakulima kupitia mazao tofauti na halimashauri kukusanya mapato yake na kujiendesha vizuri.
Aidha Mwenyekiti wa Halimashauri ya Wilaya ya Kaliua Mh Japhael Lufungija amebainisha kua mara kadhaa wananchi wa Kaliua wanashindwa kupata manufaa kulingana na uuzaji holela wa mazao kwa madalali.
“Kaliua tunalima mazao mchanganyiko ya mpunga,karanga, Mahindi, tutaenda kuyaweka kwenye mfumo nasisi kama viongozi tumeona tuwakilishe wananchi tujifunze na tukatoe elimu kwa wananchi wetu jinsi mfumo unavyoendesha ili tukalete tija kwa wakulima kwakuwa wanauhitaji katika uuzaji wa mazao“amesema Lufungija
Awali akitoa mafunzo Kaimu Mkurugenzi Halimashauri ya Wilaya ya Ruangwa Nolasco Kilumile ambae ni Afisa kilimo amesema mfumo huo hadi kuleta manufaa katika jamii unahusisha Mkulima, Msafirishaji,muendeshaji wa Ghala,amcos, vyama vikuu vya ushirika,Mnunuzi, Taasisi za fedha , pia Bodi ya zao husika pamoja na mfumo wa TMX ambao ndio unasimamia uuzaji wa mazao kwa sasa Tanzania.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa