Wataalamu kutoka TAMISEMI wametembelea na kukagua miradi ya Afya na Elimu inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa.
Ziara hiyo imefanyika leo tarehe 27/06/2022 na Miradi iliyotembelewa ni Zahanati ya kijiji cha Mbangala, Shule msingi Chiwangala, majengo ya Afya katika Hospitali ya Wilaya, madarasa ya UVIKO shule ya msingu Chunyu na Maabara mbili shule ya sekondari Mandawa.
Afisa kutoka Tamisemi Bi Joyce Kitundu alipongeza ufanisi aliouona katika usimamizi na utekelezaji wa miradi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa.
Amesema Bi Joyce kasi iliyokuwepo katika usimamizi wa miradi iendelee hivyo hivyo kwani miradi inaridhisha.
Naye Ndg Elia Erasto Malaki alisema muda uliowekwa kwa ajili ya kukamilisha miradi inayotelekezwa uzingatiwe na kuhakikisha mafundi wanajenga kwa kufuata taratibu na maelekezo yanayotolewa na Serikali.
Ndg Elia amesema miradi inaendelea vizuri hivyo uongozi usibweteke, huu ni wakati wa kuzidi kukagua miradi na kuwasimamia mafundi ili wakabidhi kazi kwa wakati.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa