Mkurugenzi mtendaji wa Wilaya ya Ruangwa Ndg: Frank F. Chonya akiongozana na DEO Msingi ndg: George Mbesigwe, Mtaalam wa ofisi ya ujenzi Eng: Noel na Mtaalam wa kutoka ofisi ya Ugavi na kushirikiana na uongozi wa kata, Mhe. Diwan kata ya Likunja na uongozi wa kijiji cha Likunja amefanya mkutano na wananchi wa Kijiji cha Likunja kata ya Likunja.
Mkutano huo uliofanyika 21 Machi 2023 atika shule ya msingi likunja, Mkurugenzi ameutambulisha Mradi wa ujenzi wa vyumba vya Madarasa 5 na ofisi 2 wenye thamani ya Shilingi Milioni.100 ambapo wananchi wametakiwa kushiriki kujitolea nguvu kazi katika hatua za awali za ujenzi wa madarasa hayo ikiwamo kuchimba msingi na kujaza kifusi.
Kwa uapnde wao baadhi ya Wananchi wameeleeza namna walivyoupokea mradi huo na kwamba utasaidia kuifanya shule hiyo kuwa ta kisasa kutokana na miundombinu iliopo sasa kuwa chakavu
Fedha zinazotekeleza mradi huo ni kutoka serikali kuu zilizotolewa na Mhe. Dkt. Samia suluhu Hasan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo katika halmashauri ya wilaya Ruangwa zinatumika kwenye ujenzi wa madarasa katika shule kongwe za msingi, miongoni mwa shule zilizonufaika na mradi huo mpaka sasa ni Shule ya msingi Nandaga kata luchelegwa na shule ta msingi Likunja , huku shule zingine zikitarajiwa kunifaika kabla ya kuisha kwa mwaka wa fedha 2023/2023.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa