• Anuani zetu |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Ruangwa District Council
Ruangwa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Uongozi wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Ardhi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Usafi na Mazingira
      • Kata
    • Vitengo
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Tehama
    • Kata
      • Nandagala
      • Mbekenyera
      • Likunja
      • Mnacho
        • Nangumbu
      • Malolo
      • Nachingwea
      • Ruangwa
      • Makanjiro
      • Mbwemkuru
      • Narungombe
      • Nangumbu
      • Luchelegwa
      • Chinongwa
      • Mandawa
      • Chunyu
      • Matambarale
      • Nkowe
      • Nambilanje
      • Nanganga
      • Namichiga
      • Mandarawe
      • Chibula
      • Chienjele
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba
  • Mradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi ya Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Videos
    • Hutuba
    • Albamu ya Picha
    • Habari
    • Tukio
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari

SERIKALI ITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI-MAJALIWA

Posted on: February 21st, 2023

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea  kuungana na wananchi katika kuimarisha miundomibu ya elimu ili kuhakikisha watoto Wakitanzania wanapata elimu bora na kutimiza ndoto zao.

Waziri Mkuu amesema kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia ameendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha watoto wanapata elimu bora kuanzia ngazi ya elimu msingi hadi chuo.

Amesema hayo leo (Februari 21, 2022) alipotembelea shule za Sekondari za Lucas Malia na Mary Majaliwa zilizopo Ruangwa Mkoani Lindi. “Rais Dkt. Samia anaweza sababu amekuwa kiongozi imara, ameendelea kusisitiza kuwa yupo pamoja nanyi.”

Waziri Mkuu amesema kuwa pamoja na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia kuweka mkazo katika kuipa hadhi sekta ya elimu, pia amewekeza kwenye elimu ya mtoto wa kike kwa kuweka sheria zitakazo muwezesha mtoto wa kike kutimiza ndoto zake

“Pamoja na kwamba Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Samia anasimamia ubora wa elimu kwa watoto wote ikiwemo wakiume, watoto wetu wa kike tumewawekea mikakati mahsusi ikiwemo sheria kali kwa wanaotaka kumkwamisha na sisi tunazisimamia ili aanze darasa ya awali mpaka  atakapomaliza akiwa salama.”

“Wazazi hii shule ni yetu, watoto ni wetu ni lazima tuwalinde na kuchangia kasi ya maendeleo katika shule hii, tuwatembelee walimu wetu ili tuwatie moyo, tunataka watoto wasome ili wafikie ndoto zao.”

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack amesema kuwa mkoa huo unatekeleza mpango mkakati ambao unafanyiwa mapitio kila mwaka ili kuona kwenye mapungufu kwa lengo la kurekebisha walipokosea na kukuza ufaulu kwa shule mkoani Lindi.

Ameongeza kuwa kupitia mpango huo wamefanikiwa kupunguza daraja sifuri kwa asilimia 40 na daraja la nne kwa zaidi ya asilimia 45. “Asilimia zaidi ya 50 ya waliomaliza mwaka jana wataenda kidato cha tano na tunauhakika mtoto aliyemalia kidato cha sita mkoani Lindi anakwenda chuo kikuu.”

Kwa upande wake, Mke wa Waziri Mkuu mama Mary Majaliwa amewataka wanafunzi hao wasome kwa bidii na wasijihusishe na makundi ovu na badala yake  waweke malengo katika masomo yao ili waweze kutimiza ndoto zao kielimu.

“Nawahusia watoto wangu someni ili muweze kupata sifa za kuwa viongozi na kuajiriwa ili muweze kuitumikia nchi yetu, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia amefanya mambo makubwa sana katika kuliinua Taifa.”

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA November 08, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAHUDUMU WA AFYA 872 KWA NGAZI YA JAMII HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA July 09, 2024
  • TANGAZO LA AJIRA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA August 01, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA March 13, 2023
  • Ona zote

Habari mpya

  • MKURUGENZI WA RUANGWA AHIMIZA USAFI NA MAZOEZI KWA AJILI YA AFYA BORA

    May 10, 2025
  • SMAUJATA YAENDESHA ELIMU DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA KWA WASICHANA RUANGWA

    May 09, 2025
  • BURIANI

    May 07, 2025
  • MHE. MAJALIWA AAINISHA MAFANIKIO MAKUBWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO RUANGWA CHINI YA UONGOZI WA RAIS SAMIA

    May 03, 2025
  • Ona zote

Video

MAENDELEO YATAKUJA KWA KULIPA USHURU, TOZO NA ADA ZA HALMASHAURI. MWANANCHI LI0A KODI KWA MAENDELEO YETU
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Mpango wa Bajeti 2017/2018(MTEF)

Kurasa zinazofanana

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • BARAZA LA MITIHANI

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Anuani zetu

    Ruangwa

    Anuani ya Posta: S.L.P 51

    Simu ya Mkononi: 0732932312

    simu: 0732932312

    Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Usiri
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa