Mgeni Rasmi katika sherehe za siku ya wafanyakazi Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi ambaye pia ni mkuu wa Mkoa wa Lindi, ametoa pongezi kwa uongozi wa Wilaya ya Ruangwa kwa zawadi nzuri kwa wafanyakazi wake.
Katika sherehe hizo, wafanyakazi bora kutoka wilaya mbali mbali walipewa zawadi zao huku kwa Wilaya ya Ruangwa kila mtumishi hodari katika idara yake alikabidhiwa pesa taslim shilingi laki nne (400,000) jambo lililopongezwa na Mkuu wa Mkoa .
Baada ya pongezi hizo Mkuu wa Mkoa amewataka watumishi wote katika nafasi zao watimize wajibu wao katika kuiletea nchi maendeleo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Andrea chezue, amewahimiza watumishi wote kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo ambayo kila mmoja katika nafasi yake amekabidhiwa
"Naomba niwapongeze wale wote mliokabidhiwa zawadi zenu leo, lakini mkumbuke kuwa kila mmoja ana wajibu wa kufanya kazi kwa bidii ili kuleta babadiliko chanya katika halmashauri yetu" amesema Mkurugenzi Andrea Chezue
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa