RAIS SAMIA-UWANJA WA MAJALIWA UTAKUWA CHACHU KATIKA KUKUZA SEKTA YA MICHEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewapongeza wananchi wa wilaya ya Ruangwa kwa ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Majaliwa.
Rais Samia amesema kuwa ujenzi wa uwanja huo utakuwa chachu katika kukuza sekta ya michezo nchini,
Ameyasema hayo leo (Jumapili, Septemba 11, 2022) alipompigia simu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa uzinduzi wa uwanja huo, katika halmashuri ya Ruangwa mkoa wa Lindi,
“Nawapongeza pia kwa sherehe nzuri ya kuzindua uwanja wa mpira wa miguu wa Majaliwa, uwanja huo pia utatumika kwa ajili ya mazoezi kwa timu zetu.”
Awali, akizungumza na Wana-Ruangwa Mheshimiwa Majaliwa amewashukuru wananchi hao kwa kuamua kuchangia shilingi 20 katika kila kilo moja ya mazao wanayoyauza ili kufanikisha ujenzi wa uwanja huo.
"Natambua mchakato wa ujenzi wa uwanja huu umetokana na mawazo yenu na matamanio yenu, hivyo mkaamua kutekeleza ili tuwe na uwanja huu. Maamuzi yenu ya kuchangia mlicho nacho yametufikisha hapa. Hongereni sana."
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amesema kwa ridhaa ya wakazi wa Ruangwa ambao wameridhia kuendelea kuboresha uwanja huo, msimu ujao wa ligi yatawekwa ili kuwezesha sehemu ya mashabiki kukaa.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa