Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa inatoa pongezi za dhati kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutimiza miaka minne ya uongozi imara uliojaa mafanikio makubwa kwa Taifa letu.
Katika kipindi hiki, Wilaya ya Ruangwa imenufaika kwa kiasi kikubwa kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwa ni matokeo ya dira na dhamira thabiti ya Serikali ya Awamu ya Sita. Kupitia uongozi wake mahiri, tumepokea Shilingi Bilioni 64,411,650,408.99/= kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya elimu, afya, miundombinu, kilimo, na sekta nyingine muhimu zinazogusa maisha ya wananchi wetu moja kwa moja.
Tunaendelea kushuhudia maboresho makubwa katika huduma za jamii, uboreshaji wa miundombinu ya barabara, ujenzi wa shule na vituo vya afya, pamoja na uwezeshaji wa wananchi kupitia mikopo na fursa za kiuchumi. Mafanikio haya ni ushahidi wa dhahiri wa dhamira ya dhati ya Serikali ya Mhe. Rais Dkt. Samia katika kuwaletea wananchi maendeleo na ustawi wa kweli.
Tunampongeza na tunamuombea afya njema, hekima, na uongozi wenye mafanikio zaidi katika kuijenga Tanzania yenye maendeleo jumuishi na ustawi kwa wote.
#kaziinaendelea
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa