Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango imeipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kwa kubuni chanzo cha mapato ambacho ni shamba la mikorosho litakalokuwa linamilikiwa na Halmashauri hiyo.
Hayo yamesemwa na kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango katika shamba la miche ya mikorosho lililopo vijiji vya Machang’anja na Nangurugai baada ya kufanya ziara yake machi 12/2018.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Rashidi Nakumbya aliupongeza uongozi wa Halmashauri hiyo kwa kazi kubwa iliyofanyika ya kusafisha na kuanza kupanda miche hiyo ya mikorosho.
“Kazi imefanyika kubwa na inaonekana kilichobaki sasa ni kukimbizana na kipindi hiki cha mvua mpande miche iliyobaki, mjitahidi mpaka wiki inayokuja muwe mmemaliza shughuli za upandaji”amesema Nakumbya
Aidha Mheshimiwa Nakumbya amesema wananchi waliopo katika eneo la shamba la Halmashauri ni watu wanaowategemea katika uangalizi wa shamba kwa kipindi hiki na kuwaomba kuwa wavumilivu wakati wanawaangali jinsi ya kutatua malalamiko yao
“Nyie ni watu muhimu sana hatuwezi kuwaacha mnanung’unika sisi kama wanakamati hii tutalichukua jambo hili na kulizungumzia sehemu husika, ila wakati mnaendelea na uchimbaji wa mashimo ya kupanda miche ya mikorosho ule ufuta mliopanda wa kule bondeni mjitahidi kuung’olea usije ukaharibika” amesema Nakumbya.
Naye Afisa Kilimo wa Wilaya Haronii Kihara alilielezea shamba hilo kwa kamati kuwa ni mkakati wa muda mrefu wa kuongeza mapato kwa halmashauri.
Kihara amesema shamba hilo linaukubwa wa ekari 1,000 ambalo halmashauri imepanga kupanda miche ya mikorosho ambayo itakuwa tayari kuvuna baada ya miaka 2.
Aliendelea kusema kutokana na ukubwa wa shamba Halmashauri imepanga kupanda ekari elf 200 kwa mwaka 2018, ambapo kila ekari moja itakuwa na miche 68 na kila mche utatoa kilo tatu za korosho wakati wa mavuno.
“Waheshimiwa Madiwani ufuta mnaouona sasa shambani hapa si wa Halmashauri bali ni wa wakulima ambao tumewapa maeneo haya bure walime kwa makubaliano ya kutulindia shamba hili hata nyie waheshimiwa mnakaribishwa kuja kulima” amesema kihara
Halmashauri imesafisha shamba kwa gharama zake ila inakaribisha wakulima kuja kulima eneo hilo ili waweze kulinda miche iliyopo shambani hapo na pia Halmashauri imetoa ajira kwani wakulima wanaolima katika eneo hilo wamepata kibarua cha kuchimba mashimo na kupanda miche.
Naye Mkulima wa Ufuta Omari Saidi aliuomba uongozi wa Halmashauri waanze kuchimba mashimo katika maeneo waliolima ufuta kabla ufuta aujajifunga na waliomba mashimo ya miche katika maeneo waliolima wapande wenyewe kwa ajili ya kutunza walichilima.
“Tunakaribia kuondoka kurudi majumbani kwetu hivyo tunaomba mashimo yaanzwe kuchimbwa huku kwenye mashamba yetu ya ufuta na tuchimbe wenyewe wasije watu wengine wakaharibu” amesema Omari.
Mwisho
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa