Naibu waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amemtaka mkandarasi wa safi campany group anaesimama mradi wa maji wa Nangumbu ambao utahudumia vijiji vya Nangumbu na Michenga kufanya kazi kwa ubora unaotakiwa ili wananchi wamaeneo hayo waweze kupata huduma na kuhakikisha suala la maji linaisha mara moja katika vijiji hivyo kwani lengo la serikali kumtua mwanamke ndoo kichwani ifikapo 2020.
Mhe. Aweso ameyasema hayo alipokuwa akikagua mradi wa maji utakaohudumia kijiji vya nangumbu na michenga wakati wa ziara yake ya kikazi katika Wilaya ya Ruangwa siku ya tarehe 05/12/2018.
Akiwa katika ziara hiyo Naibu Waziri alisema kuwa mradi wa maji wa nangumbu umetengenezwa kwa awamu mbili, awamu ya kwanza imekamilika kwa gharama za shilingi milioni 93 kutoka kwa wafadhiri na kwa awamu ya pili imeanza na utatumia gharama ya milioni 400 na fedha hizo zote zitatolewa na Serikali
Mhe Aweso ameutaka uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kutumia fedha zilizotolewa kwa ajili ya mradi kwa matumizi yaliyokusudiwa na kuhakikisha wanasimamia hatua kwa hatua shughuli zinazofanywa na mkandarasi huyo.
"
Mwisho
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa