Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Japhet Hasunga amewataka wanachi kushirikiana na serikali kuhakikisha wanatangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika mkoa wa Lindi pamoja na mikoa mingine ya kusini.
Naibu waziri ameyasema hayo leo tarehe 28/10/2018 katika sherehe ya kufunga tamasha la utamaduni la watu wa Mkoa wa Lindi lililofanyika katika kijiji cha makumbusho jijini Dar es Salaam
"Lindi ni Mkoa uliobarikiwa kuwa na vivutio vya utalii ambavyo havipatikani dunia nzima hivyo ni wajibu wa serikali kuhakikisha miundombinu inajengwe ili watalii wa Tanzania na wasio watanzania waweze kufika katika maeneo hayo".
Aidha Naibu waziri Hasunga amemuagiza Mkuu wa mkoa wa Lindi kuanzisha makumbusho ya Mkoa itakayohifadhi kumbukumbu muhimu za utamaduni ikiwa ni pamoja na kutoa elimu juu ya utamadumi wetu hata kwa vizazi vijavyo.
Pia amewataka wananchi wote kukemea vitendo vinavyofanywa na vijana haswa wasanii ambao wamekuwa wakisahau utamaduni na mila zetu kwa kufanya vitu visivyo na maadili na watumie mda wao kuenzi na kuonyesha utamaduni wetu.
Sambamba na hayo ,Naibu Waziri amezitaka halmashauri kutenga bajeti ya maadhimisho ya tamasha la Utamaduni ambalo litakuwa linaadhimishwa mwezi wa tisa kila mwaka katika kila mkoa.
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Godfrey Zambi amewashukuru wadau wote waliwaunga mkono wanalindi katika kufanikisha tamasha hilo la utamaduni wa watu kutoka Lindi.
Mwisho
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa