Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mhe. Andrew Chikongwe amezindua Kamati ya "Kasema" itakayoshirikiana na Mradi wa Elimu ya Juu kwa mageuzi ya Uchumi unaoongozwa na Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM).
Uzinduzi huo umefanyika leo Julai 9, 2024 katika Kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mwenyekiti wa Halmashauri.
Kamati ina Wajumbe watano na ina lengo la kukusanya na kushughulikia maoni au malalamiko ya wananchi katika eneo husika kuhusu Mradi.
Pia, ina lengo la kuweka kumbukumbu za kile kinachofanyika katika Mradi, na ni sehemu ya Ulinzi na Usalama wa Mradi huo.
Mradi wa Elimu ya Juu kwa mageuzi ya Uchumu chini ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam umefadhiliwa na Mkopo wa Benki ya Dunia na utekelezaji wake ni katika maeneo mapya 14, na mpaka sasa maeneo mapya matatu tayari yameshafikiwa ambayo ni Ngongo(Lindi Manispaa), Likunja( Wilaya ya Ruangwa) pamoja na Kagera.
Katika hatua nyingine, Mhe. Chikongwe ameupongeza Uongozi wa Kata ya Likunja kwa kutoa Hekari 400 ambapo Kitivo cha Kilimo kitajengwa.
Kwa upande wake, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo ambaye ni Mratibu wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa mageuzi ya Uchumu Profesa Bernadeta Killiani ametoa wito kwa wananchi wa Ruangwa kutoa ushirikiano kwani mafanikio ya Mradi itategemea muamko na ushirikiano wa wananchi wenyewe.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa