Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Hassan Ngoma ametoa wito kwa wananchi wa Wilaya hiyo kutambua thamani ya utunzaji rasilimali zao kama misitu na mito katika maeneo yao
Amesema hayo leo tarehe 30/06/2022 wakati wa kupitisha wa mpango wa matumizi bora ya ardhi katika kijiji cha Narungombe.
Amesema mpango wa matumizi bora ya ardhi ni maelekezo ya serikali na mkakati ni kila kijiji cha Ruangwa kiwe katika mpango wa matumizi bora ya ardhi.
"huu si mpango wa mkuu wa wilaya au Mkurugenzi haya ni maelekezo na sheria ipo tangu zamani na kila tutakapokuwa tunapata fedha kila kijiji kitafikiwa" amesema Ngoma
Amesema Mheshimiwa Ngoma, katika kutekeleza Mpango wa matumizi bora wananchi wa eneo husika wanapaswa kushirikishwa na kusikilizwa maoni yao wakati zoezi likiendelea.
"Huu ni mpango wa serikali hivyo ni muhimu utekelezwe ila rudini katika vitongoji vyenu mkasikilize wananchi wenu maoni yao na yafanyiwe kazi".
Naye kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Ndgu. George Mbesigwa amesema
Sasa ni muda wa kuacha kuishi kwa mazoea na kuanza kuishi kwa kufuata sheria za matumizi bora ya ardhi.
"tunapaswa kubadilika tuanze sisi na wengine watabadilika, tubadilike kifikra na tujue
Kulima katika mto ni kukausha mito. tubadilike kifikra kwasababu tumeshapewa elimu, sitegemei kuona hili jambo likitokea hapa kwetu Narungombe" amesema Mbesigwa.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa