Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mheshimiwa Hassan Ngoma ameongoza Kikao cha kwanza cha maandalizi ya kuupokea Mwenge wa Uhuru kiwilaya leo Machi 14, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Wilaya ambacho kimehusisha Wakuu wa Idara na wadau mbalimbali ambapo ameitaka Kamati inayoshughulika na ukimbizaji wa mwenge kumairisha Afya zao kwani si kazi ya lelemama.
Kwa mwaka 2024 Mwenge kitaifa utawashwa April 2, 2024 mkoani Kilimanjaro na kilele chake kitafanyika Octoba 14, 2024 mkoani Mwanza ikiongozwa na kauli mbiu " Tunza mazingira na shiriki uchaguzi wa serikali za Mitaa kwa ujenzi wa Taifa endelevu" ambapo kwa mwaka jana Wilaya ya Ruangwa ilishika nafasi ya kwanza kimkoa na kikanda na nafasi ya 13 kitaifa.
Aidha, Ngoma ametoa wito kwa wanakamati kila mmoja kutimiza wajibu wake katika nafasi yake ili kuleta tija na matokeo chanya halikadhalika ametoa pongezi kwa Kamati ya Mwenge Kata ya Nandagala na Mandawa kwa mapokezi mazuri na shughuli zote za mkesha kwa mwaka 2023.
Lakini pia kwa mwaka 2024 Mwenge utapokelewa kijiji cha Nangumbu Kata ya Malolo Wilaya ya Ruangwa na mkesha utafanyika Shule ya sekondari Mbekenyera.
Kwa upande mwingine, Mheshimiwa Ngoma amewataka wamiliki na wahudumu wa Baa na kumbi za starehe kuheshimu imani za watu kwani kipindi hiki Wakristo wapo kwenye kwarezma na Waislamu wapo kwenye Mfungo Mtukufu wa Ramadhan.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa