Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Hassan Ngoma amefanya Kikao cha kusikiliza kero za Wafanyabiashara wa Ruangwa leo Julai 12, 2024 katika Ukumbi wa Chama cha Walimu wilayani Ruangwa na kuwaahidi ya kwamba kero zao zinakwenda kutatuliwa.
" Naenda kuyafanyia kazi malalamiko yenu na ninawaahidi kuwa baada ya wiki mbili yatakuwa yamekwishwa, kwani ninajua Wafanyabiashara ndio mnaoendesha uchumi wa Wilaya, Mkoa na nchi kwa ujumla" Amesema Ngoma.
Miongoni mwa kero zilizobainishwa na Wafanyabiashara hao ni pamoja na lugha isiyo rafiki kutoka kwa Maafisa wakusanya kodi, ukadiliwaji wa juu wa kodi, mazingira yasiyo rafiki kwa ufanyaji wa biashara, kutengewa maeneo ya kutosha kwa ajili ya Wafanyabiashara ndogondogo, kuongezewa muda wa kufanya biashara, kuwepo na utaratibu mzuri wa kukata leseni, kutokuwepo kwa huduma ya vyoo yenye uhakika maeneo ya biashara
Aidha, Mhe. Ngoma ameendelea kwa kusema kuwa Taifa linaendeshwa na kodi, ila sio kodi ya machozi, jasho na damu na kitu chochote cha maendeleo kinachofanywa na Serikali basi hutokana na kodi za Wafanyabiashara.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa