Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Hassan Ngoma ameanza ziara ya Kijiji kwa Kijiji ambapo leo Agosti 12, 2024 amefanya ziara Kijiji cha Litama, Chinongwe A na B, Juhudi A na B na Likwachu vilivyopo Kata ya Chinongwe wilayani Ruangwa.
Ziara hiyo ina lengo la kusikiliza kero na changamoto mbalimbali za wananchi katika Vijiji husika.
Miongoni mwa kero na changamoto zilizobainishwa na wananchi wa Vijiji hivyo ni pamoja na upungufu wa Vyama vya Ushirika, upungufu wa huduma wa vyoo shuleni, uhaba wa Walimu, uhaba wa Mikutano ya Serikali ya Kijiji, changamoto ya wafugaji kuharibu mazao ya wakulima, changamoto ya mtandao, upungufu wa vilula vya maji, changamoto ya ugawaji wa pembejeo, changamoto ya miundombinu na changamoto ya usambazaji wa nishati ya umeme katika maeneo yote.
Kwa upande wao, Wakuu wa Idara husika walifafanua na kujibia changamoto hizo na kuwaahidi kuzitatua kwa wakati.
Katika hatua nyingine, Mhe. Ngoma atoa wito kwa wananchi wa Vijiji hivyo kushiriki kikamilifu kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 itakayoanza na kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili kupata haki ya msingi ya kuchagua viongozi bora.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa