Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Mhe. Hassan Ngoma, ameongoza kikao cha tathmini ya Mkataba wa Lishe kwa robo ya kwanza ya mwaka 2024, kuanzia Julai hadi Septemba, kikao hicho kimefanyika leo, Novemba 29, 2024, katika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa.
Kikao hicho kimehusisha wataalamu kutoka Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii, na Lishe, ambapo wamejadili utekelezaji wa shughuli za lishe katika maeneo kama utoaji wa huduma kwa wanawake wajawazito, watoto walio chini ya miaka mitano, na vijana wa umri wa balehe. Aidha, huduma za matibabu ya utapiamlo na kuzuia magonjwa yanayotokana na mtindo mbaya wa maisha zilijadiliwa kwa kina.
Wilaya ya Ruangwa imefanikisha utoaji wa elimu ya lishe kwa wazazi na walezi wenye watoto chini ya miaka miwili, kufikia walengwa 12,824 kati ya 12,824 sawa na 100%. Pia, watoto wanane walipatiwa matibabu ya utapiamlo kupitia Kituo cha Afya cha Ruangwa Mjini, huku wajawazito 6,259 kati ya 6,270 sawa na 99.82% wakipatiwa virutubisho vya Folic Acid.
Aidha, Wilaya imefungua mashine tatu za kuongeza virutubishi katika Kata za Nandagala, Nachingwea, na Mandawa ili kuimarisha afya za wakazi.
Mhe. Ngoma amepongeza juhudi hizo na kusisitiza umuhimu wa kuendelea kuboresha huduma za lishe ili kukabiliana na changamoto za afya kwa makundi mbalimbali.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa