Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack amewaombea Dua Wafanyabiashara wa Wilaya ya Ruangwa leo Julai 12, 2024 katika Kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Chama Cha Walimu Ruangwa, ikiwa ni ziara yake ya kwanza baada ya kutoka ibada ya kuhiji katika mji mtukufu wa Makka
Aidha, Mhe. Telack ametoa wito kwa Wafanyabiashara hao kufanya kazi zao kwa uadilifu na uaminifu na kuhakikisha mazingira yao ya biashara yanakuwa mazuri ili kuvuta wateja zaidi.
"Hakuna kazi rahisi, kazi rahisi ni ile ya mwenzako tu, kwahiyo boresheni mazingira yenu ya kazi kwa kuyafanyia usafi na nyinyi wenyewe kuwa na kauli mzuri za kuwavuta wateja zaidi" Amesema Mhe. Telack.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa