Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Ndugu Frank Fabian Chonya, amezindua rasmi Jarida la Afya la Wilaya hiyo leo Julai 28, 2025, katika hafla iliyofanyika Ruangwa Pride Hotel.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na wataalamu wa afya, viongozi wa Serikali, wadau wa maendeleo na wananchi, ambapo jarida hilo limeelezwa kuwa chombo muhimu cha mawasiliano, uhamasishaji na ujifunzaji katika sekta ya afya.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Ndugu Chonya amesema jarida hilo ni kioo cha kazi zinazofanywa na sekta ya afya wilayani humo, likiwakilisha taarifa muhimu, changamoto, mafanikio na dira ya mbele ya huduma za afya.
Aidha, jarida hilo linajumuisha maudhui ya kitaalamu, hadithi za mafanikio, tafiti fupi, takwimu, na mikakati ya kisekta katika kuimarisha huduma za afya kwa wananchi, hasa katika mapambano dhidi ya magonjwa ya mlipuko, huduma ya mama na mtoto na uboreshaji wa miundombinu ya afya.
Vilevile, wageni walioudhuria hafla hiyo wamesema wamefurahishwa na hatua hiyo, wakieleza kuwa ni mfano wa kuigwa kwa Halmashauri zingine nchini, na ushahidi wa dhamira ya kweli ya Serikali katika utoaji wa huduma bora za afya.
Kwa upande mwingine, Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa imeendelea kufanya maboresho makubwa kwenye sekta ya afya kwa kushirikiana na Serikali Kuu na wadau mbalimbali, ikijumuisha kuimarisha ufuatiliaji wa huduma na uwajibikaji wa watendaji katika ngazi zote.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa