Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Andrea Chezue, ameitaka Menejimeti ya Halmashauri kutoa ushirikiano wa kusimamia katika ujengaji wa ujenzi wa uwanja wa kisasa wa mpira.
Amesema hayo katika kikao kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri wakati akiongea na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri hiyo.
Amesema ni wajibu wa kila Mkuu wa Idara na vitengo kushiriki hatua kwa hatua katika shughuli za ujenzi kwani uwanja huo ni wa Halmashauri na si Mkurugenzi pekee yake.
“kuna wakuu wa idara na vitengo wanaingia moja kwa moja kutokana na idara zao msisubiri kuambiwa fanya kitu Fulani jitume na washirikishe waliochini yako ili kufanikisha lengo hili”Amesema Chezue.
Aidha Mkurugenzi amesema uwanja huo utakuwa ni chanzo cha mapato ya Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kutokana na kukodisha Hostel, kukodisha vibanda vya biashara na viingilio vya milangoni.
Vilevile amesema lengo la kujenga uwanja huu ni kuibua na kukuza vipaji vya vijana wa Ruangwa kwenye michezo mbalimbali ili kuweza kupata ajira kwani michezo kwa sasa ni ajira.
Pia kuinua kipato cha wajasiriamali ambao watapata fursa ya kufanya biashara wakati wa michezo, na jamii itapata fursa ya kuziona timu mbalimbali. Uwanja huo utatumika kwa michezo ya kitaifa na kimataifa kwasababu vipimo vyake ni vya kimataifa.
Naye Afisa Michezo wa Wilaya Simon Mwambe amesema kwasasa kazi zinaendelea wameishapeleka mchanga kwa ajili ya kufyatua tofali za kujengea ukuta katika uwanja huo.
“Tumeishachimba msingi wa kujenga ukuta, tuna saruji za kutosha na maji yapo tumefunga pampu kwenye kisima kilichochimbwa uwanjani hapo na kesho zoezi la kufyatua tofali litaanza” amesema Mwambe.
Hata hivyo Afisa Michezo amesema suala la kuazima vitendea kazi kwa watu binafsi linasababisha kuna muda kazi zisimame kwa sababu wakati vifaa vinaenda kukodiwa na muhusika anakuwa amekodisha au anatumia kwa shughuli zake.
Mwambe ametoa wito kwa vijana wa Ruangwa kujitolea kushiriki katika ujenzi wa uwanja huo kwani huo ni uwanja huo ni wakwao na ukikakamilika utakuwa na manufaa makubwa kwao zaidi.
“Huu ni uwanja wenu kama mnanafasi mje mjitolee msaidie kazi ndongondogo kwa mfano wakati niko Singida uwanja wa Namfua unajegwa kuna vijana walikuwa wanakuja kujitolea huku wakisema tumechoka kwenda kuangalia simba na yanga mbali tunataka kuangalia kwetu na kweli sasa wanaangalia Simba na Yanga Mkoani kwao Singida”amesema Afisa Michezo.
Mradi huu utakapokamilika unakisiwa kutumia kiasi cha billion 2.5, na kazi zilizofanyika mpaka sasa zinathamani ya Tshs 148,204,000/= na kiasi cha fedha ambacho kimelipwa hadi sasa Tshs 50,640,000/=.
MWISHO.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa