Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Hassan Ngoma amekabidhi pikipiki 20 kwa vikundi vitatu vya vijana vinavyokopeshwa na halmashauri kwa kupitia mapato ya ndani ikiwa ni mkopo wa Vijana wanawake na walemavu.
Amekabidhi mikopo hiyo tarehe 19/05/2022 ofisini kwa Mkuu wa Wilaya Ruangwa mjini.
Wakati anakabidhi mkopo huo Mheshimiwa Ngoma alisema vijana waliopokea mkopo huo wanatakiwa kujua mkopo waliokopeshwa wanatakiwa kulipa kwa wakati.
"Hizo pikipiki si msaada mnapaswa mlipe kwa wakati ili wengine nao waweze kunufaika na mikopo hiyo zingatieni mikataba inavyotaka"amesema DC
Vile vile aliwakumbusha kufuata sheria za barabarani na kutunza pikipiki hizo ili iweze kudumu na iweze kuendelea kuwaingizia kipato.
Pikipiki zikizokopeshwa ni 20 kwa vikundi vitatu vya Mtakulini cha Chinongwe, Fursa cha Ruangwa na Juhudi cha Mbekenyera zenye jumla ya shilingi millioni 57,132,000.
Mkopo huo ni Mwaka mmoja ambapo kila wiki kwa pikipiki moja inatakiwa kurudisha shilingi elf 55000 katika akaunti ya Wanawake, Vijana na watu wenye Ulemavu banki ya CRDB
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa