Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Ndugu Frank Fabian Chonya, amekabidhituzo kwa Mhasibu wa Halmashauri hiyo, Joseph Mdasia Maheke, leo tarehe 21 Julai 2025, kama ishara ya kutambua mchango na uchapakazi wake katika utumishi wa umma.
Tukio hilo limefanyika katika kikao cha kawaida cha Menejimenti ya Halmashauri (CMT) kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mkurugenzi, ambapo viongozi na wakuu wa idara wameshuhudia na kushiriki kumpa pongezi Mhasibu huyo kwa utendaji wake bora.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mkurugenzi Chonya ameleza kuwa Maheke ameonesha weledi, uaminifu na bidii kazini, mambo ambayo yanapaswa kuwa mfano kwa watumishi wengine. Amesisitiza kuwa Halmashauri itaendelea kuwatambua na kuwathamini watumishi wanaotekeleza majukumu yao kwa uadilifu na ufanisi.
“Madasia ameonesha kiwango cha juu cha uwajibikaji, uaminifu na bidii kazini.
Halmashauri inatambua na kuthamini watumishi wanaoweka juhudi na uadilifu katika kazi zao, tunataka hili liwe somo na motisha kwa wengine.” amesema Chonya.
Kwa upande wake, Mdasia ameshukuru kwa tuzo hiyo na kueleza kuwa imempa nguvu mpya ya kuendelea kuhudumu kwa moyo wa uzalendo, kufanya kazi kwa bidii zaidi kwa manufaa ya wananchi wa Ruangwa na maendeleo ya taifa kwa ujumla.
“Ninashukuru sana kwa kutambuliwa. Tuzo hii si yangu peke yangu, bali ni ya timu nzima tunayoshirikiana nayo kila siku, naahidi kuendelea kuwajibika kwa uaminifu na bidii zaidi.” amesema Mdasia.
Hata hivyo, Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Uhasibu CPA Goodluck Bernard Swai amepongeza juhudi na mwenendo mzuri wa Mdasia, akimtaja kuwa mfano wa kuigwa katika suala la maadili, weledi na kujituma. Amesisitiza kuwa utambuzi kama huu huongeza morali kazini na kuchochea maendeleo ya taasisi kwa ujumla.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa