• Anuani zetu |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Ruangwa District Council
Ruangwa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Uongozi wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Ardhi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Usafi na Mazingira
      • Kata
    • Vitengo
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Tehama
    • Kata
      • Nandagala
      • Mbekenyera
      • Likunja
      • Mnacho
        • Nangumbu
      • Malolo
      • Nachingwea
      • Ruangwa
      • Makanjiro
      • Mbwemkuru
      • Narungombe
      • Nangumbu
      • Luchelegwa
      • Chinongwa
      • Mandawa
      • Chunyu
      • Matambarale
      • Nkowe
      • Nambilanje
      • Nanganga
      • Namichiga
      • Mandarawe
      • Chibula
      • Chienjele
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba
  • Mradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi ya Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Videos
    • Hutuba
    • Albamu ya Picha
    • Habari
    • Tukio
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari

MAONESHO YA MADINI LINDI 2025 YAHITIMISHWA KWA MAFANIKIO MAKUBWA RUANGWA

Posted on: June 14th, 2025

Maonesho ya Madini na Fursa za Uwekezaji Mkoa wa Lindi 2025 yamefungwa rasmi leo tarehe 14 Juni katika Viwanja vya Maonesho Kilimahewa, Wilayani Ruangwa.


Tukio hilo kubwa limefungwa na Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Dkt. Steven Kiruswa (Mb.) kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ruangwa.

Akizungumza wakati wa kufunga maonesho hayo, Mhe. Dkt. Kiruswa ameeleza kuwa Serikali itaendelea kusimama bega kwa bega na wachimbaji wadogo na wawekezaji wa ndani na nje ili kuhakikisha rasilimali za madini zinawanufaisha wananchi wote.


“Tunapenda kuona wananchi wa Lindi na Tanzania kwa ujumla wakifaidika moja kwa moja na rasilimali hizi. Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na kuwezesha wachimbaji wadogo kupiga hatua zaidi,” amesema Dkt. Kiruswa.


Kwa upande mwingine, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Zainab Telack, amewapongeza waandaaji, wadau, na wananchi kwa kujitokeza kwa wingi, akisisitiza kuwa maonesho hayo ni sehemu ya mapinduzi ya kiuchumi kwa Mkoa wa Lindi.


“Lindi siyo tena Mkoa wa kusubiri, sasa tunasonga mbele kwa vitendo. Maonesho haya yamedhihirisha kuwa tunaweza kujenga uchumi imara kwa kutumia fursa zetu za ndani, hususan katika madini,” amesema Mhe. Telack.

Aidha, kwa siku nne mfululizo (11–14 Juni), zaidi ya mabanda 120 yaliwekwa na kuendeshwa na wachimbaji wadogo, taasisi za umma, mashirika binafsi, wajasiriamali na watoa huduma mbalimbali katika mnyororo wa thamani wa sekta ya madini.


Mbali na hayo, mwaka huu maonesho yaliambatana na kauli mbiu:

“Madini na Uwekezaji: Fursa ya Kiuchumi Lindi – Shiriki Uchaguzi Mkuu 2025.”


Vilevile, zaidi ya asilimia 75 ya uendeshaji wa maonesho uligharimiwa na wadhamini wakubwa kama Ellianje Genesis, Lindi Jumbo, MAST, UVIWAMA, PMBet, pamoja na makampuni, taasisi na watu binafsi zaidi ya 50.


Kwa ujumla, Kwa ujumla, maonesho haya yametoa dira mpya kwa uchumi wa mkoa, kuleta hamasa kwa wachimbaji wadogo, na kuongeza mwamko wa wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA 17.11.2025 November 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA March 13, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI April 25, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III August 09, 2023
  • Ona zote

Habari mpya

  • HOSPITALI YA WILAYA YA RUANGWA YAPATA USAJILI KWA MAFUNZO ENDELEVU YA KITAALUMA (CPD)

    November 20, 2025
  • MHE NGOMA AWAPONGEZA NMB KWA KUIPANDISHA THAMANI YA KOROSHO KWA WANANCHI WA RUANGWA

    November 18, 2025
  • MAADHIMISHO YA SIKU YA LISHE KITAIFA 2025

    November 15, 2025
  • MAAFISA UTAMADUNI WAKUTANA NA WALAMBO, NGARIBA NA WAMILIKI WA VIWANJA VYA JANDO NA UNYAGO

    November 14, 2025
  • Ona zote

Video

MAENDELEO YATAKUJA KWA KULIPA USHURU, TOZO NA ADA ZA HALMASHAURI. MWANANCHI LI0A KODI KWA MAENDELEO YETU
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Mpango wa Bajeti 2017/2018(MTEF)
  • Watumishi Portal

Kurasa zinazofanana

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • BARAZA LA MITIHANI

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Anuani zetu

    Ruangwa

    Anuani ya Posta: S.L.P 51

    Simu ya Mkononi: 0732932312

    simu: 0732932312

    Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Usiri
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa