Maelfu ya wananchi wa Wilaya ya Ruangwa wamefurika katika Kiwanja cha Wandorwa kusherehekea kwa shangwe na furaha kuupokea mwaka mpya wa 2025.
Tukio hilo limekuwa la kipekee likisindikizwa na burudani mbalimbali, ikiwemo muziki wa moja kwa moja, michezo ya utamaduni, na hotuba za viongozi wa jamii waliohimiza mshikamano na amani kwa mwaka mpya.
Hali ya shangwe imetawala kutoka kwa wananchi wa rika mbalimbali waliokusanyika kwa wingi kushiriki tamasha hilo la kihistoria, wengine wameeleza kuwa hafla kama hii inachangia kuimarisha mahusiano ya kijamii na kuhamasisha maendeleo ya pamoja.
Wananchi wamepongeza maandalizi ya hafla hiyo, huku wakielezea matumaini ya mwaka mpya kuwa wa mafanikio zaidi kwa Wilaya na Taifa kwa ujumla.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa