Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za mikoa na Serikali za mitaa Mhe. Innocent Bashungwa ametoa wito kwa watumishi wa umma kutumia fedha za umma kwa kufuata kanuni na taratibu zinazowekwa.
Amesema fedha zote zinazotolewa kwa ajili ya kutekeleza miradi zina maelekezo yake hivyo wataalamu wafuate maelekezo hayo.
Amesema hayo leo tarehe 29/06/2022 katika hafla ya kumpongeza Mheshimiwa Rais Samia Suluhu iliyofanyika viwanja vya ILulu Lindi Mjini.
"fedha zikitumiwa vizuri miradi itakamilika kwa wakati na wananchi watapata huduma bora kwa wakati".
Aidha aliwataka wakurugenzi kuendelea kusimamia vyema ukusanyaji wa mapato katika halmashauri zao.
"Wananchi wetu ni waelewa si wabishi kulipia ushuru hivyo simamieni ukusanyaji wa mapato katika kila sekta" amesema Bashungwa
Mhe waziri alitumia hadhara hiyo kuwaasa wananchi kujiandaa na zoezi la sensa na kuwapa ushirikiano makarani wanapopita kutelekeza zoezi hilo. Tushiriki zoezi la sensa ili iwe rahisi kuletewa huduma za kijamii kwa ufasaha.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa