Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa wameonyesha kuridhishwa na juhudi za dhati ambazo zimekuwa zikionyeshwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Andrea Chezue kwa namna ambavyo amekuwa bega kwa bega kwa kushirikiana na madiwani pamoja na timu nzima ya menejimenti katika kuhakikisha rasilimali za Halmashauri zinatumika kadri ipasavyo na kuleta tija kwa wananchi.
Hayo yamebainishwa Juni 9 mwaka huu na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mhe. Rashid Nakumbya alipokuwa akifungua baraza la madiwani na kusema kuwa kwa nyakati tofauti tofauti Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa imekuwa na wakurugenzi mbalimbali lakini kupitia Mkurugenzi Chezue wanayo mambo ya kujivunia katika usimamizi wa miradi mbalimbali ambapo rasilimali zimekuwa zikitumika vizuri na kuleta tija katika miradi ya maendeleo inayoendelea maeneo mbalimbali na kuleta tija kwa wananchi.
Pia ameitaka menejiment ya wilaya kuendelea kufanya shughuli zake kama zamani kipindi hiko ambacho madiwani watakuwa nje na kutokwamisha shughuli za kimaendeleo.
“Wawekezaji wanapofika msiwakwamishe kusiwe na masharti mengi na masuala la mikataba na vibali ishighulikiwe kwa uharaka bado tunaimani na nyie na tunajua hamtotuangusha kwa kipindi hiki ambacho tupo nje” amesema Nakumbya.
Naye Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa ndg, Andrea Chezue amesema kama Mkurugenzi na timu ya menejimenti wamekuwa wakipata ushirikiano mkubwa kutoka kwa madiwani ambao wamekuwa chachu ya kufanya vizuri kwa kuhakikisha miradi yote iliyoko katika kata zao inasimamiwa na kufanyika katika ubora stahiki jambo lililosaidia Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kuwa mfano wa kuigwa ama chuo cha kujifunza kwa wilaya nyingine ambapo asilimia kubwa ya miradi hiyo imekuwa ikifanyika kwa ubora na thamani stahiki
“Ruangwa yasasa ni Ruangwa ya kimaendeleo tulipo hapa ni ushirikiano mliotupatia waheshimiwa Madiwani Nimejifunza mengi kwa kufanya kazi na baraza lako mwenyekiti mlivyoiacha Halmashauri basi mtaikuta salama”amesema Chezue
Pamoja na hayo Chezue amewatia moyo madiwani hao na kusema kuwa ni maombi yake kuona madiwani hao wakirejea tena madarakani kwa kipindi kingine ili waweze kuliendeleza mbele gurudumu la maendeleo huku akiahidi kuendelea kufanya kazi zake kwa juhudi kwa kuhakikisha usalama wa rasilimali hususani fedha hadi hapo madiwani watakaporejea tena madarakani na kwamba kasi ya miradi ya maendeleo itaendelea kama kawaida na kwamba kazi zitaendelea kufanyika kwa uadilifu mkubwa kwa kuweka alama za maendeleo katika Wilaya ya Ruangwa.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa