Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi wamefanya Uchaguzi wa kumchagua Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ambapo Mhe. Mikidadi Mbute Diwani wa Kata ya Namichiga ameshinda Uchaguzi huo kwa kupata kura 26 za Wajumbe kwa kipindi Cha mwaka wa fedha 2024/2025.
Uchaguzi huo umefanyika leo Agosti 14, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa.
Katika uchaguzi huo wagombea walikuwa wawili mmoja kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na chama Cha ACT Wazalendo ambapo mgombea kutoka Chama Cha Mapinduzi alikuwa Mhe. Mikidadi Mbute na kutoka ACT Wazalendo alikuwa Mhe. Rose Nyenela.
Akitangaza matokeo ya Uchaguzi huo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndugu George Mbesigwe akieleza kuwa wajumbe waliotakiwa kupiga kura ni 29, kura halali zilizopigwa zilikuwa 26 na wajumbe watatu hawakupiga kura kutokana na hali hiyo Mhe. Rose Nyenela alipata kura 0 na Mhe. Mikidadi Mbute alipata kura 26 hivyo Msimamizi wa uchaguzi alimtangaza Mheshimiwa Mikidadi Mbute kutoka Chama Cha Mapinduzi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Wakati huo huo Madiwani walichagua Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Halmashauri kwa kipindi cha mwaka 2024/2025.
Kwa upande wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji Mwenyekiti aliechaguliwa ni Mhe. Rashidi Lipei, Diwani wa Kata ya Mandawa.
Kamati ya Uchumi, ujenzi na Mazingira Mwenyekiti wake ni Mhe. Shabani Kambona, Diwani wa Kata ya Nanganga na Mhe. Jafari Mwambe, Diwani Kata ya Malolo alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili.
Mkutano huo ulikuwa wa robo ya nne ya mwaka wa fedha wa 2023/2024 hivyo ulikuwa wa kufungia mwaka.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa