Madini yenye ubora aina ya kinywe yabainika katika Wilaya ya Ruangwa, madini hayo ni kati ya madini mkakati kumi na moja ya dunia katika vitalu vinavyomilikiwa na Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Hayo yamebainishwa na Mjiolojia Mwandamizi kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa madini (GST) kutoka ndg.Charles Moye akizungumza katika kikao cha baraza la Halmashauri kilichofanyika leo tarehe 14/09/2021 alisema madini hayo kiubora viwango vyake vimevuka wastani wa ubora unaohitajika kimataifa.
Amesema "Na kwa upande wa majibu sampuli za miamba zilizokusanywa na kupimwa kiwango cha Carbon (TGC %) zilionyesha kiwango hicho kilianzia asilimia 4% mpaka asilimia 18% kiwango cha juu na sampuli nyingi kuwa na wastani wa TGC 12% ambacho ni kikubwa ukilinganisha na kiwango cha ubora wa madini ya hayo ya kinywe duniani ambacho ni 3%
Mjiolojia huyo amebainisha kuwa eneo hilo linafaa kwa uwekezaji wa madini hayo hivyo ni fursa nzuri ya wawekazaji na wachimbaji wadogowadogo kufanya makubaliano na Halmashauri ili kutumia eneo hilo.
Vile vile mjiolojia Ambaliche alishauri halmashauri kutumia taarifa ya utafiti iliyoandaliwa na GST katika kuhamasisha na kuvutia wawekezaji katika eneo la mradi
Aidha Ndg Moye aliishauri Halmashauri kufanya uchunguzi wa kina wa madini mengine yanayopatikana katika eneo kutokana na ukubwa wa eneo hilo.
Vile vile Ndg, Moye alisema utafiti huo ulibainisha uwepo wa madini ya manganizi katika vitalu hivyo ambayo yanahitaji ufuatiliaji zaidi
Vitaru hivyo vipo katika Kata Nambilanje ya kijini cha Nanjaru.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa