Kutokea Wilayani Ruangwa, Mkoa wa Lindi, Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia imewafikia wanafunzi wa Shule ya Sekondari Luchelegwa iliyopo Kata ya Luchelegwa leo Februari 20, 2050.
Katika kampeni hiyo, wanafunzi wamepewa elimu kuhusu haki za mtoto, ukatili wa kijinsia, wajibu wa mtoto na masuala mengine ya kisheria ili kuwajengea uelewa wa namna ya kutambua na kutetea haki zao.
Kampeni hiyo imebeba kauli mbiu isemayo “Msaada wa Kisheria kwa Haki, Usawa, Amani na Maendeleo”.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa