Kiongozi mwa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2024 Ndugu Godfrey Mnzava ameweka jiwe la Msingi Shule ya Sekondari Michenga iliyopo kijiji cha Michenga Kata ya Malolo Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi leo Mei 28, 2024 yenye thamani ya shilingi zaidi ya Milioni 560 za Kitanzania.
Shule ina vyumba vya madarasa 8, Maabara 3 na jengo la utawala ambayo imekuwa mwarobaini kwa wanafunzi ambao walikuwa wanalazimika kutembea umbali mrefu zaidi ya kilomita 20 kwenda na kurudi kutoka Kijiji cha Michenga hadi Kijiji cha Nangumbu ili kupata elimu aidha shule imepanda miti 215 katika kuhakikisha wanahifadhi mazingira ya shule.
Aidha Ndugu Mnzava atoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa Serikali za mitaa ili kuchagua viongozi sahihi na kutunza amani na usalama katika maeneo yao katika kipindi cha uchaguzi na kwa wale viongozi wayakaochaguliwa kuwapa ushirikiano katika majukumu yao ya kazi.
Pia, amewataka wananchi katika shughuli zao za kila siku kutunza mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa