Wakulima Wilayani Ruangwa wameaswa kushiriki utekelezaji wa Dhamira ya kufikia na kufanikisha mpango wa serikali wa kuwa na nchi yenye uchumi wa viwanda.
Aliwataka wananchi kuongeza bidii katika sekta ya kilimo ambayo itapelekea kuwa na viwanda kwa wingi kwasababu kilimo na viwanda ni vitu viwili vinavyotegemeana.
Wito huu aliutoa Mkimbiza Mwenge Kitaifa Amour Hamad, Amour wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nandalaga alipotembelea shamba la alizeti na kiwanda cha kukamua mafuta hayo ya alizeti.
Alisema wakulima wanawajibu wa kushiriki kikamilifu wa kuifanya nchi kuwa na uchumi wa viwanda kupitia sekta ya kilimo.
Alibainisha kwamba idadi kubwa ya wakazi wa Wilaya ya Ruangwa humo ni wakulima, hivyo wananafasi ya kushiriki mpango huo wa serikali kupitia kazi wanayofanya, Amour alifananua kuwa ili wakulima waweze kufanikisha azima hiyo wanapaswa kubadilisha mtazamo na fikra kutoka kwenye kilimo cha kawaida na kwenda kwenye viwanda.
`` Badala ya kuuza mazao ghafi wakulima wanapaswa kufikiria kuuza yaliyotengenezwa viwandani, kwa kufanya hivyo mtakuwa mmeongeza thamani mazao mnayozalisha``alisema Amour.
Aidha alisema kama Tanzania ikifanikiwa kuwa nchi ya viwanda basi kutakuwa na faida nyingi kama kuongeza ajira ya mtu mmojammoja, kukuza uchumi wa taifa na kubadilisha mfumo wa maisha kutoka katika hali duni mpaka kuwa na hali nzuri kimaisha.
``Lengo nikuona hadi kufika mwaka 2025 wananchi wameondoka kwenye lindi la umasikini nakufikia uchumi wa kati ila kufanikiwa katika suala la viwanda inabidi wananchi wakazane kufanya kilimo kwa wingi``alisema Amour.
Vilevile alimtaka Mkuu wa Wilaya kuweka mkakati wa kuzuia matumizi mabaya ya chandarua kwasababu wananachi wanabadili matumizi ya chandarua badala ya kufunga kwenye vitanda vyao wanafunga kwenye bustani zao. Hivyo aliwataka wananchi kuwa na fikira za kubadilika na si kuishi kwa mazoea.
Wakati huo huo Fredirick Joseph Ndahani alitoa pongezi kwa uongozi wa Wilaya kwa mapokezi mazuri waliyoyapata na kusisitiza Halmashauri kuongeza jitihada za kusaidia vikundi vya wajasiriamali na hasa vijana.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa