Kufuatia mwendelezo wa Jukwaa la pili la maendeleo ya ushirika Mkoa wa Lindi 2024, Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Bi. Zuwena Omary kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa amezindua na kuweka jiwe la Msingi katika kituo cha malipo ya Wakulima leo June 4, 2024 kilichopo Lipande wilayani Ruangwa.
Kituo hicho ni msaada kwa Wakulima kwani kitawasaidia kupata stahiki zao za mazao karibu yao na ni kwenye ofisi yao maalum ukilinganisha na hapo awali ambapo walikuwa wanapata stahiki zao kutoka ghala kuu.
Kituo hicho kimegharimu zaidi ya Milioni 100 za kitanzania mpaka kukamilika kwake.
Aidha Mhe. Zuwena Omary amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Hassan Ngoma kuhakikisha kampeni ya upandaji miti inaendelea katika maeneo mbalimbali wilayani humo ili kupambana dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi halikadhalika kupendezesha na kuipamba Wilaya.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa