Kwa mujibu wa Takwimu za Matokeo ya Sensa ya watu na makazi 2022 Kata ya Nachingwea wilayani Ruangwa inaongoza kuwa na idadi ya watu wengi ikiwa na watu 18,343 ikifuatiwa na Kata ya Mbekenyera yenye watu 16,531, Kata ya Nandagala ikiwa na watu 7391, huku Kata ya mwisho ikiwa ni Makanjiro yenye watu 4002 na kufanya Wilaya ya Ruangwa kuwa na julma ya watu 185,573.
Aidha, Matokeo ya Sensa ya watu na makazi imeonesha uwiano wa watu kwa jinsia idadi ya Wanaume kwa kila Wanawake 100 ambapo kwa Wilaya ya Ruangwa ina uwiano ya Wanaume 97 kwa kila Wanawake 100.
Na katika Kata za Wilaya ya Ruangwa Kata inayoongoza kwa kuwa uwiano wa juu wa jinsia kati ya Wanaume na Wanawake ni Kata ya Mbwemkuru, Machang'anja,Nambilanje, Mbekenyera, Matambarare na Chibula na hii inaonesha kwamba Wanaume ni wengi kuliko Wanawake.
Kata ya Namichiga na Chienjele uwiano wa jinsia kati ya Wanaume na Wanawake ni 100 kwa 100 na Kata ya Nandagala uwiano wa jinsia ni Wanaume 93 kwa Wanawake 100, na Kata ya Mnacho ina uwiano mdogo wa watu kwa jinsia kwa kuwa na Wanaume 91 kwa Wanawake 100.
Katika upande wa Idadi ya Kaya katika Wilaya ya Ruangwa ina jumla ya Kaya 60931 na Kata ambayo inaongoza kwa idadi kubwa ya Kaya ni Kata ya Nambilanje ambayo inaongoza kwa wastani mkubwa wa watu kwa Kaya ina wastani wa watu 3.5, Mbwemkuru wastani wa watu 3.3, Nandagala wastani wa watu 3.0 na Mnacho wastani wa watu 2.8.
Sensa ya watu na makazi 2022 aidha imeonesha idadi ya watoto chini ya umri wa miaka 18 ambapo kwa Wilaya ya Ruangwa ina 37% ya watoto chini ya miaka 18.
Na Kata inayoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watoto chini ya miaka 18 ni Kata ya Nambilanje 40.3%, Mbwemkuru 40.0%, Nandagala ina 35.6%, na Mbekenyera ina 34.4%.
Takwimu za idadi ya Vijana kuanzia umri wa miaka 15-35 katika Wilaya ya Ruangwa ni 34.6% ambapo Kata ya Nachingwea inaongoza kuwa na vijana wengi zaidi ya 40.9%, Mbekenyera ni 38.5%, Nandagala ni 33.6% na Malolo ina asilimia ndogo ya Vijana ambayo ni 30.4 ukilinganisha na Kata zote wilayani humo.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa