Washauri wa Kampuni ya Carbon First wakiongozwa na Bi. Lilian Rushango wamefanya mazungumzo na Viongozi wa vijiji vya Chingubwa, Mchichili, Nahanga na Mtondo wilayani Ruangwa.
Mazungumzo hayo yamefanyika leo Julai 16, 2024 katika Ofisi za vijiji hivyo na yalihusisha maswali kutoka kwa washauri wa kampuni hiyo na maoni ya Viongozi wa vijiji kuhusu jinsi ya kuilinda na kuitunza misitu ya vijiji hivyo kabla ya kuanza biashara ya hewa ukaa katika Wilaya ya Ruangwa.
Kwa upande wao, washauri wa kampuni ya Carbon First wamewashukuru Viongozi wa vijiji kwa ushirikiano wao na kuwaahidi kuwa maoni yao watayafanyia kazi kwa ajili ya kuboresha na kufanikisha biashara hiyo.
Nao, Viongozi wa vijiji wamefurahia ushirikishwaji huo uliofanywa na Kampuni ya Carbon First na kuona ni hatua nzuri ya kufanikisha biashara hiyo katika misitu ya vijiji vyao.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa