Kutokea Wilaya ya Ruangwa, Mkoani Lindi, Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia imewafikia wananchi wa Kijiji cha Nandanga, Kata ya Luchelegwa, leo Februari 20, 2025, wananchi wamepatiwa elimu kuhusu sheria za ndoa, ardhi, mirathi, ukatili wa kijinsia na haki zao za msingi.
Vilevile, kampeni hiyo imewezesha kutatua changamoto mbalimbali za kisheria zilizokuwa zikiwakabili wananchi kwa muda mrefu kwa kuwapa ufafanuzi wa kina. Wananchi wa Nandanga wameipongeza Serikali kwa jitihada hizo, wakisema elimu waliyopewa itawasaidia kujua haki zao na kuimarisha mshikamano ndani ya jamii.
@katiba
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa