Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) ya Ruangwa imekutana leo Februari 5, 2025, kujadili na kutoa ushauri kuhusu mipango ya maendeleo ya Wilaya, ikiwemo bajeti ya mwaka mpya wa kiserikali, kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
DCC inajumuisha viongozi wa Wilaya, wataalamu wa sekta mbalimbali, wawakilishi wa taasisi na wadau muhimu wanaoshiriki katika kupanga na kushauri kuhusu matumizi ya rasilimali kwa maendeleo ya Wilaya.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Mhe. Hassan Ngoma, amesisitiza umuhimu wa ubunifu na uwajibikaji kwa wataalamu wa sekta zote katika kuhakikisha mipango ya maendeleo inatekelezwa kwa ufanisi.
Aidha, kikao hicho kimeangazia vipaumbele vya bajeti ya Wilaya kwa mwaka mpya wa fedha, huku wajumbe wakitoa maoni yao kuhusu mbinu bora za usimamizi wa rasilimali.
Washiriki wa kikao hicho wameelezea dhamira yao ya kuhakikisha ushauri unaotolewa unaleta matokeo chanya kwa ustawi wa wananchi wa Ruangwa.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa