Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa ambae ni Afisa Elimu Awali na Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Ndugu George Mbesigwe amewataka walimu wote wa shule husika kujaza Takwimu ili kupata taarifa zilizo sahihi.
Ameyasema hayo leo April 02, 2024 katika Kikao cha ufunguzi wa Semina ya maelekezo ya ujazaji wa madodoso ya sensa ya Elimu Msingi kilichofanyika ukumbi wa Shule ya Sekondari Nkowe.
Kikao hicho kimehusisha Maafisa Elimu Kata, Walimu Wakuu, Wakuu wa shule, Walimu wa Takwimu na Maafisa kutoka Ustawi wa jamii wenye vituo vya kulelea watoto wadogo.
Aidha, Mbesigwe ametoa wito kwa Maafisa Elimu Kata kusimamia kiyakinifu zoezi la ujazaji wa Takwimu kwa Walimu ili kuendana na wakati na kuhakikisha walimu wanamaliza mitaala yao mapema ili kuwasaidia wanafunzi kupata muda mwingi wa kupitia yale waliyofundishwa ili kupata matokeo mazuri pindi wafanyapo mitihani.
" Kama mwalimu anza kwa kusema sisi ni kichwa na si mkia hii itasaidia kujitafakari wapi ulianguka mwaka uliopita na kufanya kilicho bora mwaka husika kwa kufundisha kwa weledi tena kwa kuzingatia muda ili kumaliza mitaala mapema" Amesema Mbesigwe
Kwa upande wao wadau waliohudhuria Kikao hicho wamewaomba wahusika wa usajili wa vituo vya kulelea watoto wadogo kushirikiana kwa pamoja na wadau wanaowiwa kufungua vituo hivyo ili vituo hivyo vitambulike mapema na serikali halikadhalika wameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kwa kuinua na kuitolea macho Sekta ya elimu.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa