Katibu wa Chama cha Wafanyakazi Serikali za Mitaa Mkoa wa Lindi (TALGWU),Ndg Jafari Ndande, amewataka watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kukusanya mapato na kuona ni wajibu wao kulinda mapato ya halmashauri yasipotee.
Amesema hayo wakati wa kikao cha baraza la bajeti la wafanyakazi lililifanyika tarehe 02/02/2022 katika ukumbi wa Mkuu wa Wilaya Ruangwa mjini.
Ndugu Ndande alisema kuacha mapato yapotee itasababisha mateso kwa watumishi wenyewe kwasababu Halmashauri haitoweza kutoa stahiki za watumishi.
"Suala la kukusanya mapato ni wajibu wa kila mtumishi msikae katika vituo vyenu vya kazi mkifikiri suala la mapato ni la mkurugenzi tu hapana ni wajibu wenu wote watumishi wa Halmashauri hii" amesema
Vile vile alisema kila mtumishi akiwa na mawazo ya kuwa fedha hizo zikipotea zinapotea zake hakutokuwa na mapato yanayopotea ya wilaya hii na Mkurugenzi ataweza kukamilisha stahiki zote za watumishi.
Naye kaimu Mkurugenzi Ndgu Albert Mwombeki alisema ni wajibu wa kila mtumishi kulinda vyanzo vyote vya mapato na kuhakikisha mapato hayapotei.
Alisema Mwombeki mipango yote ya halmshauri iliyopangwa kwenye bajeti itafanikiwa kama kila mtu atatimiza wajibu wake katika kukusanya mapato ya halmashauri.
" msiruhusu mapato yapotee ~msiruhusu watu~ wala kuibwa simamieni vyanzo vya mapato na hakikisheni kila mzigo inayotoka katika kata na vijiji vyenu vimelipiwa ushuru" amesema Mwombeki
Katika kikao hicho Baraza la Wafanyakazi lilipotisha bajeti ya billion 30.8 ya mwaka 2022/2023 ikiwa mapato ya ndani ni billion 5.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa