Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa ametoa wito kwa wananchi wa Kijiji cha Namahema B kilichopo Kata ya Nandagala wilayani Ruangwa kufanya kazi kwa bidii hususani kwenye kilimo ili kutimiza ndoto zao.
"Hakuna namna ya kubadili maisha yetu kama si kujiimarisha na kujituma kiuchumi, wapo watu wengi wamefanya mambo ya maendeleo kupitia kilimo, tusikidharau kilimo, cha msingi ni kulima kisasa kwani kwenye maisha hakuna mafanikio ya miujiza ni lazima ufanye kazi ndipo ufanikiwe" Amesema Chikongwe.
Ameyasema hayo leo Julai 12, 2024 katika Kikao kazi kilichohusisha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Viongozi wa Kata ya Nandagala, Viongozi wa Kijiji cha Namahema B, Viongozi wa Benki ya NMB na Wakulima wa bustani za mbogamboga kutoka Kata ya Nandagala na Mnacho kilichofanyika katika kijiji cha Namahema B.
Aidha, Mhe. Chikongwe amewaomba wananchi wa Kijiji cha Namahema B, kuhakikisha mazingira ya maeneo wanayoishi yanakuwa safi ili kujikinga na magonjwa yanayotokana na uchafu, pia amewataka kufikiria na kubuni biashara mbalimbali ili kuwavutia wawekezaji na kufanya kijiji kinachangamka kimaendeleo.
Kwa upande wake mkulima wa bustani za mbogamboga kutoka kijiji cha Ng'au kilichopo Kata ya Mnacho Ndugu Nelson Sweetbert ametoa pongezi kwa viongozi wa Kata ya Nandagala na kuahidi kuyafanyia kazi kwa vitendo yale waliyoagizwa.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa