Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe, Hassan Ngoma amewataka Viongozi wa Halmashauri na Serikali ya kijiji wanaosimamia zoezi la ugawaji pembejeo za ruzuku ya Viwatilifu kwa ajili ya korosho kufuata haki na usawa katika zoezi la ugawaji pembejeo hizo.
Amesema hayo wakati wa mapokezi ya pembejeo hizo katika ghala la Chama Kikuu Runali lililopo kijiji cha Lipande Ruangwa.
Alisema pembejeo hizo haziwezi kumtosha mkulima hivyo ni wajibu wa mkulima kuongeza idadi ya pembejeo katika shamba lake kama hitaji lake lilivyo.
"Kuhudumia shamba lako ni wajibu wako mkulima ila Serikali imeamua kukusaidia kukupatia pembejeo bure baadhi hivyo zinazobaki kanunue mwenyewe" amesema Ngoma
Pia aliwataka wananchi wafahamu kuwa pembejeo hizo zimeletwa na Serikali kwa lengo la kuwagaiwa wananchi bure hivyo ikitokea mtu anaambiwa atoe fedha ndiyo apaewe pembejeo atoe taarifa polisi haraka.
" Tutapita kukagua hadi kwenye maduka mfanyabiashara tukikukuta na pembejeo hizi za ruzuku tutakuchukulia hatua za kisheria" amesema Ngoma
Mapokezi ya awamu ya kwanza kwa salfa tani 60, ubwiri unga na braiti boksi 2460 na kiua wadudu lita 866 na zoezi la ugawaji litaanza tarehe 31/05/2022
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa