Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango imemtaka fundi uashi aliyejenga mabweni katika shule ya sekondari Nkowe afanye marekebisho ya frem za milango alizoziweka katika mabweni mapya yanayojengwa katika shule hiyo.
Kauli hii imetokana na baada ya kamati kufanya ziara yake kama ilivyoada na kugundua kuna madhaifu makubwa katika uwekaji wa fremu za milango katika upande wa mabweni.
Hayo aliyasema wakati wa ziara ya kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango iliyofanyika tarehe 16/10/2017, Ziara hii ilijumuisha waheshimiwa madiwani pamoja na wataalamu kutoka Halmashauri.
Mhe Mwenyekiti wa Halmashauri Rashidi Nakumbya alisema majengo yanayojengwa katika shule hiyo ni mazuri ila watu wachache wanaweza kuyafanya yakawa hayana mvuto unaotakiwa.
“Serikali inafanya mambo mazuri ya kusaidia kutoa misaada kama hiyo inapaswa siye tunaopewa tuitende haki kwa kujenga kwa ustadi unaotakiwa ili tuweze kuwa na sifa na vigezo vya kupata mikopo mingine”alisema Nakumbiya.
Vile vile kamati hiyo ilimuagiza mhandisi wa maji kwenda katika kijiji cha michenga kuongea na serikali ya kijiji na wananchi kiujumla kueleza mambo yote yanayohusiana na mradi wa maji uliopo katika kijiji cha Michenga.
“Serikali ya sasa ni ya uwazi sana hivyo ni muhimu wananchi wetu kujua kila kitu kinachohusu na kinachoendelea katika mradi huu wa ufadhili wa Japan”alisema Nakumbya.
Wakati huo Mwenyekiti wa Halmashauri aliutaka uongozi wa kamati ya ujenzi katika shule ya Sekondari Ruangwa ikajifunze katika kata zingine wanafanyaje kazi zao katika kuwashirikisha wananchi na mpaka wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo.
Mwenyekiti alisema Wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo ya maeneo yao ni jambo la msingi na umuhimu hivyo nawaagiza muitishe kikao cha wazazi muweze kujadiliana jinsi watakavyotia nguvu zao kwa namna moja.
“Maeneo mengi yameamka sasa hivi wananchi wake wanajitoa sana katika kutia nguvu zao ili kuendeleza shughuli za kimaendeleo zinazofanyika katika maeneo yake sasa nashangaa hapa mjini bado watu hawan amuamko katika hilo inapaswa muwashirikishe kuanzia sasa”alisema Nakumbiya.
Katika ziara hii kamati ilitembelea miradi mbalimbali ambayo ni Mradi wa ujenzi Radio Ruangwa, Ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari Ruangwa, Ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari Kassim Majaliwa,Ujenzi na ukarabati wa kituo cha Afya Nkowe, Ujenzi wa vyumba vya madarasa na mabweni shule ya sekondari Nkowe, Ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Michenga na Mradi wa maji katika kijiji cha Nangumbu.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa