Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mheshimiwa Hashim Mgandilwa amewataka wakazi wa Ruangwa kuendelea kujiunga mfuko wa jamii (CHF) iliyokuwa inatumika mwanzo ya shilingi 15,000 wakati wakiendelea kusubiri kuletewa CHF iliyoboreshwa ya shilingi 30,000.
Amesema hayo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Mandarawe katika vijiji vya Nandeje, Nachinyimba na Mandarawe Leo 10/10/2018 .
Amesema Mheshimiwa Mgandilwa CHF iliyoboreshwa itakuwa ni nzuri sana kwani inawafanya mpate matibabu ndani ya Mkoa kwa watu 6 watu wazima wawili na watoto waliochoni ya miaka 18 wa nne hivyo itakapofika mjiunge kwa wingi kuepusha gharama kubwa za matibabu ukiwa ndani ya Wilaya na nje ya Wilaya.
"Mie nawaonea huruma wananchi wangu wa Ruangwa ndiyo maana nawasisitiza mjiunge na CHF kwasababu unalipia shilingi 15,000 kwa mwaka na mnapata matibabu watu 6 sasa kwanini mmalize pesa kwa kila siku kwenda kutibiwa na kulipia matibabu, CHF ni mkombozi wenu" asema Mheshimiwa Mgandilwa.
Aidha amewataka wananchi hao kuacha kufanya unyago kwa watoto wao kipindi cha muhula ya masomo na waelewe kuwa serikali inaheshimu mila na tamaduni ila shughuli hizo zifanywe wakati wa likizo za mwezi wa sita na kumi na mbili ili kuwapa watoto wao fursa ya kupata elimu ikiwa ni haki yao ya msingi.
"Nitoe onyo kwenu yoyote atakayefanya shughuli za unyago wakati wa masomo pamoja na kufanya vigodoro nitamshughulikia, fanyeni unyago kipindi kilichokubalika lakini sio vigodoro." amesema Mgandilwa.
Naye bi Asha Mapua alisema wao wataendelea kujiunga na CHF ya zamani kama Mkuu wa Wilaya alivyowataka Ile serikali ingefanya haraka kuwaletea CHF iliyoboreshwa kwani wanaisubiri kwa hamu.
Pia Mzee Huruma Hemedi aliwaomba wananchi kufuata maagizo ya Mkuu wa Wilaya ya kuzingatia muda wa kufanya unyago ambao unapaswa kufanyika.
Alisema elimu ni kitu muhimu hivyo ni wajibu wao kufuata mitaala ya elimu na watazingatia hilo ili kukuza kiwango cha ufaulu katika shule zote za Wilaya ya Ruangwa.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa